Jumanne, 4 Oktoba 2016

    PICHA: Tingatinga Lilivyofukua mamilioni yaliyokuwa Yamefichwa ardhini


     

     
    Kama wewe unadhani huna fedha, basi kuna wengine ambao wamezichimbia ardhini, tena kwa mamilioni. Benki ya chini ya ardhi iliyosheheni mamilioni ya fedha, zilizoswekwa ndani ya mifuko myeusi ya plastiki na kufukiwa mchangani, imechimbuliwa na matrekta ya kutengeneza barabara jijini Arusha huku noti nyekundu zikitawanywa kila kona na kufanyika kuwa 'Sadakalawe - Amina,' kwa kila mpita njia ambaye angeweza kujitwalia fungu.

    Ilikuwa ni mshikemshike katika eneo la Mianzini mjini Arusha , ambako kuna mradi mkubwa wa upanuzi wa barabara ya kutoka Mianzini Mataa hadi Ilkiding'a unaoendelea.

    Watu walipigana vikumbo katika harakati za kujineemesha na fedha zilizokuwa zimetapakaa eneo hilo. Ikiwa imesheheni noti tupu, tena nyekundu na mpya, kufumuliwa kwa akaunti hiyo ya benki ya chini ya ardhi pamoja na kuwa neema kwa wapita njia na wakazi wa eneo hilo, kuligeuka pia kuwa kilio kwa mmiliki wa hazina hiyo, Christopher Akoonay maarufu kama 'Mmbulu' ambaye sasa amejipatia jina jingine la 'Mabulungutu.'

    Akonaay ni mkulima, lakini hasa akijishughulisha na ufugaji wa ng'ombe wa maziwa. Yeye hudamka asubuhi kukamua mifugo hao na kisha kusambaza bidhaa hiyo ya maziwa katika maeneo mengi ya jiji katika kuwauzia wakazi wa Arusha.

    Na katika siku ya tukio, Akonaay alikuwa yuko kwenye shughuli zake za kuwapelekea maziwa wateja wake, ndipo watengeneza barabara walipofika eneo hilo la Mianzini na tingatinga zao na kuanza kuichimba njia hiyo ya kutoka Mianzini hadi Ilkiding'a katika kata ya Ilboru, inayotenganisha Jiji la Arusha na wilaya ya Arumeru.

    Ikiwa imejengwa kwa fito na matope, nyumba ya 'Mmbulu' ilikuwa miongoni mwa zile zilizobomolewa na ni baada ya wamiliki wake, kugoma kuzibomoa wenyewe ili kupisha upanuzi wa barabara hiyo.

    “Shauri letu tulilipeleka mahakamani kudai fidia kabla ya mradi wa barabara haujapita hapa,” alisema Akonaay na kuongeza kuwa mara baada ya kesi yao kutupiliwa mbali na chombo hicho cha sheria, wajenzi hawakusubiri hata saa moja ipite, bali walikwenda moja kwa moja eneo hilo na kuanza kazi.

    Baadhi ya wakazi wa Mianzini, wakizungumzia suala hilo kwa masharti ya kutotajwa majina, walisema ni ajabu kwa Mzee Akonaay kuwa na kiasi kikubwa cha fedha na kuzifukia ardhini huku mwenyewe akiishi kwenye nyumba duni ya matope.

    Lakini Akonaay ambaye kwa sasa anaitwa 'Mabulungutu,' anasema kuwa alikosa imani na benki maana wakati akifanya kazi serikalini miaka ya 1980, alifungua akaunti na akawa anaweka fedha zake zote benki.

    Baada ya kustaafu mwaka 1994 na kuamua kushughulika na ufugaji, hakuzifuatilia tena fedha zake benki hadi mwaka 2000, ambako alipokwenda kuangalia fedha zake aliambiwa kuwa kwa sababu akaunti yake haikuguswa kwa zaidi ya miaka 10, alitakiwa aende Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kujieleza. Hata hivyo, aliona huo ni usumbufu na kuamua kuanza kuweka fedha zake nyumbani.

    Lakini hii pia ilimtokea puani baada ya mmoja wa ndugu zake kuzikwapua zote mara baada ya kuzifuma katika vitita vyenye thamani ya Sh milioni 20 na zaidi. Sasa Akonaay akaja na mkakati mpya wa kuhifadhi fedha kwa kuchimba shimo katikati ya chumba chake cha kulala, kilichokuwa upande wa barabara ya Mianzini na kuanza kuweka hazina yake humo.

    Lakini tena, bahati mbaya ikiendelea kumuandama, makatapila ya wachonga barabara, yakaifukua benki yake hiyo ya ardhini na kutawanya fedha zaidi ya Sh milioni 35 zilizoishia kuokotwa na wapita njia pamoja na majirani, ambao kwa hofu hawakupenda hata kulizungumzia sakata hilo.
     


    Jumatatu, 26 Septemba 2016

    Ukifanya Haya Mambo Mapenzi Yatanoga Kwa Asilimia 90




    Wanaume wengi hupuuzia hili, huona kama ni jambo lisilo na maana sana kwao na wenzi wao. Hali ni tofauti sana kwa wanawake ambao hupenda kuwasifia wanaume zao. Nitakupa mifano miwili ya namna wanandoa wa jinsia mbili tofauti wanavyotambulishana kwa jamaa zao. Kwa mafano manakutanata kwenye majumuiko ya harusi na sherehe kama hizo. Mme 1 akamtambulisha mkewe kwa jamaa zake, huyu ni mama Rick mke wangu. Mme wa 2 akamtambulisha mkewe, huyu ni my lovery sweetheart wife, nampenda sana kuliko wanawake wote duniani. Kama upo kwenye huu utambulisho umeona tofauti gani? hao wanawake wa pande mbili watajisikiaje? Nahisi umejifunza kitu hapo

    MALENGO SHIRIKISHI
    Wanaume wengi wana ulemavu mmoja; hawapendi kuwashirikisha wanawake katika mambo yao. Wanapenda kufanya mambo yao kwa siri na wakati mwingine ikilazimika kumwambia mkewe basi kwa mshtukizo baada ya kukamilisha jambo husika. Siku hizi dunia imebadilika, kuna mambo mengi. Kuna suala la hasara katika biashara, utapeli, kifo cha gafla, ajali n.k. Mkeo ndiye rafiki yako mkubwa kuliko wote, ndiye ndugu yako wa karibu zaidi kuliko yeyote. Mmeshirikiana kuzaa watoto na kujenga maisha pamoja. Yeye anapaswa kujua mambo yako, ndiye mtetezi wako nambari wani. Mweleze juu ya malengo yako, wakati mwingine anaweza kukusaidia sehemu ambayo hukutarajia. Hata hivyo, kumshirikisha katika malengo yako, kunampa nguvu na nafasi ya kujiona mama katika familia yenu. Lakini ngoja nitoe angalizo, kuna wanawake ambao huwezi kumshirikisha from A to Z ya malengo yako kutokaa na tabia na mienendo ya maisha, hope kila mtu anafahamu strength and weakness ya wake na waume zetu, so be careful in some extent.

    KIPAUMBELE/CONCERN
    Kuna wakati wanawake huwa na mambo yao binafsi. Kazini au kifamilia. Inawezekana akatatizika katika eneo fulani ambalo kwa namna moja ama nyingine atahitaji usaidizi wako. Ikitokea mkeo akawa katika hali hiyo, msikilize. Mathalani ana tatizo la kifamilia, amekuambia mmoja wa wazazi wake anaumwa, msaidie. Si lazima kifedha, lakini kuonesha kujali kwako tu, kutampa matumaini na faraja kwamba anaishi na mtu sahihi. Acha kupuuza mambo yake; hata yale madogo, kama ya ‘mtoto wa dada amerudishwa ada shuleni’. Msikilize, mshauri panapofaa kufanya hivyo na ukiweza msaidie hata kifedha. Katika upande wa pili ni hivyo hivyo. Labda una tatizo binafsi, kikazi au kifamilia, mshirikishe. Unaweza kushangaa jambo ambalo uliamini unaweza kulimaliza peke yako, kwa kumshirikisha likawa jepesi zaidi na mambo yakaenda vyema. Kipaumbele kwa namna yoyote ile, kunaongeza mapenzi zaidi kwa mwanamke.
    "Together we swim in the same pool"

    USAFI
    Asilimia kubwa ya wanawake wanapenda sana usafi. Ni aghalabu kukutana na mwanamke asiyejipenda. Ndiyo maana wanaitwa mapambo ya nyumba au ua la nyumba! Ni kwa sababu ya hulka yao ya kupenda sana usafi. Mwanamke anavutiwa sana na mwanaume mtanashati. Usafi wako unamfanya ajiamini kuwa na wewe. Hata nyumbani kwako, lazima uishi katika nyumba safi. Hata anapokuja kukutembelea, anakuta mazingira masafi kuanzia sebeleni hadi chumbani. Anapokukuta katika hali ya usafi, inakuwa rahisi zaidi yeye kuanzia hapo alipokukuta na kuendelea mbele. Rafiki yangu, kama uko mbali na usafi, ujue kuwa itakuwa vigumu kupata mdada wa ukweli – yule wa ndoto zako. Wanaume wengine wanapanga kutoka outing na wapenzi wao, mkifika huko mwanamke anajuta WHY amekubali kukutana na wewe maana utamkuta mwanaume hajapasi Tshirt/shirt, kwapa linapumua, ukiongea mdomo unatoa harufu inakuwa tabu tupu. Mwanume ukijipenda unatakuwa mtanashati tu

    KUJIAMINI
    Mwanamke anajisikia salama zaidi akiwa na mwanaume ambaye anajiamini – mwenye uwezo wa kutetea hoja zake na kujieleza sawia. Siyo anayebabaika. Suala la msimamo binafsi, kwa mwanamke ni kubwa kuliko hata kumnunulia manukato mapya! Mathalani unakuwa naye katika mtoko, angependa kukuona ukiwa katika hali halisi ya maisha yako, usiyeyumbishwa na mwenye kutoa maamuzi yasiyoyumba. Wakati mwingine, mwanamke anaweza kukupima hata katika jambo ambalo amekosea yeye, ataangalia unavyotoa maamuzi yako, lakini pia atafuatilia kuona kama utakuwa mwepesi wa kuyabadilisha. Anataka kuona msimamo wako muda wote. Mwenye kujiamini na mawazo yasiyo na matege wala makengeza! Usiyebadilika kama kinyonga! "Men believe on your standing hills"

    ANAYEJALI na KUFUATILIA
    Wanawake wanapenda sana wanaume wanaowajali. Wanaowaona wao ni kila kitu na wanaotoa kipaumbele kwao. Kama huna tabia hiyo, ujue upo katika nafasi kubwa ya kumkwaza mpenzi wako. Mjali mpenzi wako kwa kila hali lakini pia uwe na kiasi. Kumjulia hali kila wakati na kutaka kujua maendeleo yake, kutakupa nafasi kubwa ya kuendelea kudumu katika uhusiano hai. Wanaume wengi ni wavivu, si tu kuwatumia hata SMS za “mambo dia?” wapenzi wao lakini hata kujibu tu, “niko poa, Si hulka ya wanaume kutumatuma SMS – inajulikana, lakini angalau ukiweza kulifanya hili hata kidogo tu hata mara moja kwa wiki, utakuwa unajiongezea pointi kwa mwenzi wako na kumpa courage ya kufurahia mapenzi ya ndoa.

    MAANDALIZI YA TENDO LA NDOA
    Tendo la ndoa halina maana ya kukomoana. Jenga mazoea ya kufanya maandalizi kamili kabla ya tendo. Sikiliza hisia za mwenzako. Ukiweza kumjulia mke wako katika eneo hili, ni wazi kwamba utazidisha upendo wake kwako, lakini pia atakuwa katika kuta za uaminifu. Unapokuwa kazini mchokoze "aisee nasikia hamu leo" hayo ndo maandalizi ya saikolojia. kupitia sms hiyo utasikia feeling zake, ataji-express. Kufikia jioni/usiku utashangaa unashikwa mkoni kupelekwa kitandani. Akatafute nini nje wakati wewe ndiye mganga wake unayeweza kumtibu barabara? Jiamini katika shughuli, fanya mazoezi ya viungo hata kukimbia ili uongeze pumzi ya kutoa dozi kitandani.
    Epuka mapenzi ya kubakana, unafika tu bed unamvuta unamvua na kuanza kupanda kifuani......nooooooo hapo hakuna maandalizi ya kisaikolojia wala ya kimwili, hii itampekea kuchukia tendo because there is no any enjoyment

    OUTING SOMETIMES
    Kulingana na budget yako, si vibaya mara moja kumtoa mpenzi wako outing walau mara moja ndani ya miezi sita hata mwaka kama budget ni shida. Kwa wale wenye familia unaweza toka mkaspend 1 or 2 days outing na mkeo. Kuna mambo mmeo/mkeo anaogopa kukufanyia kulingana na mazingira ya hapo nyumbani na familia kwa ujumla. Lakini mkitoka nje LAZIMA mta-experience the difference for SURE. Pia ni njia mojawapo ya kuboresha na kupalilia penzi lenu na kuongeza uaminifu kati yenu

    Naomba niishie hapo kwa leo

    Faida za Kufanya Mapenzi Mara Nyingi Hizi Hapa...



     Watafiti wa Kizungu wanakesha kufanya tafiti chungu mzima na zingine majibu yake zinaweza kukuacha mdomo wazi.

    Kwa mfano huu – jamaa eti wamebaini kuwa kushiriki tendo la ndoa mara nyingi kunaongeza imani ya kiroho na hata imani kwa Mungu! Makubwa..

    Kwa mujibu wa utafiti, tendo la ndoa hutoa homoni ya upendo iitwayo oxytocin ambayo haiishi tu kutengeneza ukaribu wa kijamii bali pia imani ya Mungu – hususan kwa wanaume.

    Watafiti katika chuo kikuu cha Duke cha North Carolina, wanasema kuwa tendo hilo huhamasisha imani – ama kuongeza imani katika Mungu na dini.

    Utafiti huo umeliochapishwa mwishoni mwa wiki unaangalia homoni ya oxytocin ambayo huamshwa zaidi wakati wa kufanya mapenzi, wakati wa kuzaa na wakati wa kunyonyesha.

    Kutana na Mtangazaji Mchafu Zaidi Duniani


     Raphael Tenthani inasemekana kuwa ndiye mtangazaji mchafu zaidi kutokea duniani

    Raphael mara zote utakazo kutana nae huwezi ukamkuta nadhifu , mara kwa mara utamkuta amevaa nguo zilizo chakaa na muda mwingine nguo zenye matobo au viraka

    Raphael ingawa ni mwandishi wa habari katika shirika la habari la BBC nchini malawi lakini kwenye suala la usafi yeye limemkalia kushoto sana ,wakati mwingine unaweza ukakutana nae nywele hajachana, viatu vimeachama , mdomo unanuka na mara kwa mara anakuwa katika hali ya ulevi

    Raphael amekuwa gumzo sana katika mitandao ya kijamii huku wengi wakimuhisi huenda anafanya hivyo ili asivunje masharti ya mganga

    Ni kawaida kumuona Raphael akirusha habari akiwa mchafu bila kujali mahali husika alipo kuwepo.

    Meneja wa Diamond Athibitisha Kuwa ni Kweli Diamond Kanunua Nyumba Afrika Kusini..Ataja Bei Aliyolipia


     Kuna nyumba ilikuwa sokoni inayofanana na ile Diamond amedai kuinunua South, zinafanana tu ama ni ile ile? Hilo ni swali ambalo hadi sasa wengi wamekuwa wakijiuliza, lakini sasa Bongo5 ina jibu la uhakika.

    Wiki iliyopita Diamond Platnumz alitengeneza vichwa vya habari baada ya kupost kwenye Instagram picha ya nyumba anayodai ameinunua nchini Afrika Kusini itakayotumiwa na mchumba wake Zari.

    Picha hiyo aliisindikiza na maelezo mazito yaliyowalenga wale aliowaelezea kama wanaopenda kujisifia ni matajiri na kumuita yeye maskini ilhali watoto wao bado wanaishi kwenye nyumba za kupanga. Wengi walitafsiri kuwa dongo hilo lilimlenga ex wa Zari, Ivan anayefahamika kwa kuishi maisha ya kifahari.

    Hata hivyo, muda mfupi baada ya Diamond kuweka picha hiyo, wametokea watu ambao wamesambaza picha ya nyumba nyingine inayofanana kwa karibu asilimia 100 na nyumba ile iliyowekwa kwenye mtandao wa privateproperty.co.za na hivyo kuzusha minong’ono mingi.

    Kwa mujibu wa meneja wa Diamond, Sallam, nyumba hiyo imelipiwa Alhamis iliyopita na tayari ni mali ya muimbaji huyo wa Salome na amefafanua kwanini bado haijatolewa kwenye tovuti hiyo.

    “Nyumba imelipiwa thursday haiwezi toka muda huo huo kwenye website mpaka agency amalizane na mwenye nyumba then process zote zikamilike ndio inatolewa kwenye site,” Sallam ameiambia Bongo5.

    Nyumba hiyo ipo Moreleta Park, mjini Pretoria.


    Ina vyumba vitano, lounge 3, mabafu matatu, bwawa la kuogelea, balcony, gereji mbili na nyumba ya pembeni ya kuishi wafanyakazi.

    Watendaji wasimamishwa kazi

    WATENDAJI watatu wa vijiji katika wilayani ya Manyoni mkoa wa Singida, wamesimamishwa kazi kutokana na kushindwa kusimamia miradi iliyopo kwenye vijiji vyao na kusababisha upotevu wa fedha za serikali.

    Akizungumza
    na waandishi wa habari, Mkuu wa wilaya hiyo, Geofrey Mwambe, alisema amefikia hatua hiyo baada ya kutembelea vijiji hivyo mwezi huu na kukutana na upotevu wa fedha kwenye miradi mbalimbali ikiwamo ya maji huku wengine wakiwa hawajui wajibu wao katika utekelezaji wa majukumu yao.

    Aliwataja kuwa ni mtendaji wa kijiji cha Chikuyu, Msemembo na Rungwa na kwamba pia ameivunja kamati ya maji ya kijiji cha Chikuyu.


    Alisema baadhi ya miradi hiyo ni wa maji wa kijiji cha Chikuyu ambao mitambo yake inatumia sola, lakini kwenye akaunti una Shilindimilioni moja wakati mradi wa maji Soliya unaoendeshwa mitambo ya aina hiyo, lakini una zaidi ya Sh. milioni 40 kwenye akaunti.


    Alisema watendaji hao hawawajibiki ipasavyo kuisimamia miradi ya aina hiyo na kusababisha serikali kupoteza mamilioni huku wengine wakiendeleza vitendo vya rushwa.


    Alisema viongozi watendaji katika wilaya hiyo wasioendana na kauli ya Rais John Magufuli ya “hapa kazi tu” ni bora wajitoe wenyewe ili kupisha viongozi wawajibikaji wanaoweza kuwajali wananchi kwa maendeleo ya Taifa.


    Akizungumzia kuhusu maeneo ya wazi yaliyovamiwa, Mwambe alisema mpango alionao ni kuhakikisha maeneo yote ya umma yanajengewa uzio na kuwekewa alama kwa ulinzi zaidi.


    “Maeneo ya umma yalivamiwa kutokana na kutokuwapo kwa bikoni zinazoonyesha kuwa ni mali za umma,” alisema.


    Alisisitiza kama kuna kiongozi aliuza maeneo hayo ya umma kwa watu binafsi, atachukuliwa hatua za kisheria na kuirudisha mali ya umma.

    Alhamisi, 1 Septemba 2016

    RAIS JOHN MAGUFULI KUBADILISHA FEDHA



    Katika kilekinachoonekana kutaka kuwadhibiti watu wanao daiwa kuficha fedha, Rais John Magufuli amesema kwa mamlaka aliyonayo anaweza kuamua kubadilisha fedha ili zile znazofichwa na watu hao wakose mahali pakuzipeleka.



    Akizungumza katika mkutano wa 14 wa mwaka wa waandisi ulio fanyika katika ukumbi wa mlimani city leo mchana mjini DAR ES SALAM, Magufuli amesisitiza kuwa kauli hiyo nimahususi kwa watu walio ficha fedha katika majumba yao na kuwataka kuwachana na tabia hiyo mara moja ili fedha hizo ziingie katika mzunguko.


    Huku akisisitiza kuwa katika utawala wake fedha za bure hazitakuwepo kwa sababu zilizokuwepo awali zilitokana na fedha za wizi kutoka serekalini ambazo kwa sasa zimezibitiwa, alisem kwa mwendo anaokwenda nao sasa ni ngum kwa mwananchi kupata fedha bila kufanya kazi.