Kuna nyumba ilikuwa sokoni inayofanana na ile Diamond amedai kuinunua
South, zinafanana tu ama ni ile ile? Hilo ni swali ambalo hadi sasa
wengi wamekuwa wakijiuliza, lakini sasa Bongo5 ina jibu la uhakika.
Wiki iliyopita Diamond Platnumz alitengeneza vichwa vya habari baada ya
kupost kwenye Instagram picha ya nyumba anayodai ameinunua nchini Afrika
Kusini itakayotumiwa na mchumba wake Zari.
Picha hiyo aliisindikiza na maelezo mazito yaliyowalenga wale
aliowaelezea kama wanaopenda kujisifia ni matajiri na kumuita yeye
maskini ilhali watoto wao bado wanaishi kwenye nyumba za kupanga. Wengi
walitafsiri kuwa dongo hilo lilimlenga ex wa Zari, Ivan anayefahamika
kwa kuishi maisha ya kifahari.
Hata hivyo, muda mfupi baada ya Diamond kuweka picha hiyo, wametokea
watu ambao wamesambaza picha ya nyumba nyingine inayofanana kwa karibu
asilimia 100 na nyumba ile iliyowekwa kwenye mtandao wa
privateproperty.co.za na hivyo kuzusha minong’ono mingi.
Kwa mujibu wa meneja wa Diamond, Sallam, nyumba hiyo imelipiwa Alhamis
iliyopita na tayari ni mali ya muimbaji huyo wa Salome na amefafanua
kwanini bado haijatolewa kwenye tovuti hiyo.
“Nyumba imelipiwa thursday haiwezi toka muda huo huo kwenye website
mpaka agency amalizane na mwenye nyumba then process zote zikamilike
ndio inatolewa kwenye site,” Sallam ameiambia Bongo5.
Nyumba hiyo ipo Moreleta Park, mjini Pretoria.
Ina vyumba vitano, lounge 3, mabafu matatu, bwawa la kuogelea, balcony, gereji mbili na nyumba ya pembeni ya kuishi wafanyakazi.
Jumatatu, 26 Septemba 2016
Meneja wa Diamond Athibitisha Kuwa ni Kweli Diamond Kanunua Nyumba Afrika Kusini..Ataja Bei Aliyolipia
About Unknown
Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.