Watendaji wasimamishwa kazi
WATENDAJI watatu wa vijiji katika wilayani ya Manyoni mkoa wa
Singida, wamesimamishwa kazi kutokana na kushindwa kusimamia miradi
iliyopo kwenye vijiji vyao na kusababisha upotevu wa fedha za serikali.
Akizungumza
na waandishi wa habari, Mkuu wa wilaya hiyo, Geofrey
Mwambe, alisema amefikia hatua hiyo baada ya kutembelea vijiji hivyo
mwezi huu na kukutana na upotevu wa fedha kwenye miradi mbalimbali
ikiwamo ya maji huku wengine wakiwa hawajui wajibu wao katika
utekelezaji wa majukumu yao.
Aliwataja kuwa ni mtendaji wa kijiji cha Chikuyu, Msemembo na Rungwa na
kwamba pia ameivunja kamati ya maji ya kijiji cha Chikuyu.
Alisema baadhi ya miradi hiyo ni wa maji wa kijiji cha Chikuyu ambao
mitambo yake inatumia sola, lakini kwenye akaunti una Shilindimilioni
moja wakati mradi wa maji Soliya unaoendeshwa mitambo ya aina hiyo,
lakini una zaidi ya Sh. milioni 40 kwenye akaunti.
Alisema watendaji hao hawawajibiki ipasavyo kuisimamia miradi ya aina
hiyo na kusababisha serikali kupoteza mamilioni huku wengine
wakiendeleza vitendo vya rushwa.
Alisema viongozi watendaji katika wilaya hiyo wasioendana na kauli ya
Rais John Magufuli ya “hapa kazi tu” ni bora wajitoe wenyewe ili kupisha
viongozi wawajibikaji wanaoweza kuwajali wananchi kwa maendeleo ya
Taifa.
Akizungumzia kuhusu maeneo ya wazi yaliyovamiwa, Mwambe alisema mpango
alionao ni kuhakikisha maeneo yote ya umma yanajengewa uzio na kuwekewa
alama kwa ulinzi zaidi.
“Maeneo ya umma yalivamiwa kutokana na kutokuwapo kwa bikoni zinazoonyesha kuwa ni mali za umma,” alisema.
Alisisitiza kama kuna kiongozi aliuza maeneo hayo ya umma kwa watu
binafsi, atachukuliwa hatua za kisheria na kuirudisha mali ya umma.
About Unknown
Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.